Baada ya kushiriki mbio za The Great Ruaha Marathon Julai 5, 2025 ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha, Kamishna wa Uhifadhi TANAPA CPA (T) Musa Nassoro Kuji alimefanya kikao kazi na Maafisa na Askari wa hifadhi hiyo katika ofisi za Makao Makuu (Msembe).
Kikao kimelenga kuhimiza uwajibikaji, mshikamano na ari ya kazi kwa watumishi wa hifadhi hiyo kubwa zaidi katika mfumo wa Ikolojia wa Ruaha-Rungwa, wenye wanyamapori kama Tembo, Twiga, Simba, Chui, Tandala na Nyati.
Kamishna Kuji amewapongeza watumishi kwa kushiriki mbio hizo, akieleza kuwa mbali na burudani, ni jukwaa muhimu la kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji ikiwemo Mto Ruaha Mkuu.
Amesisitiza kuwa mafanikio ya uhifadhi yanahitaji jitihada za pamoja, nidhamu ya kazi na moyo wa kujitoa, akiwataka waendelee kuwa mstari wa mbele kulinda na kusimamia maliasili kwa ajili ya kizazi kijacho.
Kamishna amehimiza bidii, ubunifu na ushirikiano ili kufanikisha uhifadhi endelevu na kuwa mfano kwa jamii kwa kuonesha uwajibikaji, uaminifu na ushupavu.\n\nKamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Godwell Meing’ataki, Mkuu wa Kanda ya Kusini, alimkaribisha Kamishna Kuji na kueleza mikakati ya hifadhi katika kujenga ushirikiano na jamii jirani kupitia elimu ya uhifadhi, miradi ya maendeleo na vikundi vya uzalishaji mali.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Abel Mtui, Mkuu wa Hifadhi, amesema kuboreshwa kwa miundombinu ya utalii kumeiwezesha hifadhi kupokea watalii wengi na kuongeza mapato mwaka 2024/2025 kupitia huduma kama Game drive, Walking safaris, Balloon safaris, Bush meals, Night game drive, Sportfishing na utalii wa boti.
Ziara ya Kamishna Kuji imehusisha pia ukaguzi wa miradi ya REGROW kama uwanja wa ndege Msembe, kituo cha taarifa kwa wageni (VIC) na nyumba za kulala wageni (Cottages).
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments