MKURUGENZI wa jiji la Arusha,John Kayombo amevitaka Klabu na vyama vya michezo kuwasilisha mipango kazi yao ili waweze kusaidika.
Ameyasema hayo wakati wa kufunga bonanza la michezo la Sabasaba ambayo ilifanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Baraa iliyopo Moshono kwa kuandaliwa na timu ya Mwangaza Veterans ambapo aliwakilishwa na afisa michezo na utamaduni jiji la Arusha, Benson Maneno.
Ambapo amesema ofisi yake imejipanga kuweza kuzisaidia timu na vyama ambazo zitakuwa tayari kupeleka mipango kazi yao kwa ajili ya faida ya michezo jijini Arusha.
Amesema wamejipanga kuhakikisha Arusha inapiga hatua katika michezo ikiwemo kuwa na timu ya Ligi Kuu na kuifanya kurejesha heshima yake kama zamani ilipokuwa na timu za AFC,977KJ FC,Palsons FC ambapo kwa kuanza wameanza na ujenzi wa uwanja wa Soka ambayo inajengwa New Arusha City.
“Tuko tayari kushirikiana na mdau yeyote ambaye yuko kuwekeza katika michezo na niwaombe Klabu na vyama leteni mipango kazi yenu ofisi yangu itakuwa tayari kutoa ushirikiano”.
Katika hatua nyingine jiji la Arusha imeweka wazi kuwa itashirikiana na timu ya Mwangaza Veterans kuboresha uwanja wa Shule ya Sekondari ya Baraa ili kutoa nafasi ya vijana na wazee kushuudia burudani.
Uwanja huo utafanyiwa maboresho kataika sehemu ya kuchezea (pitch) lakini pia uwekaji wa taa ambayo itatoa nafasi ya michezo kufanyika usiku ,pia itaifanya Baraa kuwa shule ya kwanza jijini Arusha kuwa na uwanja wenye taa.
“Viongozi wa Mwangaza mje jumanne tuone namna gani tunaifanyia kazi suala ili la kuboresha uwanja ili kutoa nafasi ya soka kuchezwa”.
Haruni Kidungu ni katibu wa Mwangaza Veterans alisema kama mpango wao wa kufanyia maboresho uwanja wa Baraa utafanikiwa basi itatoa fursa kwa wadau wa michezo Arusha kuweza kushuudia burudani ya soka kutoka kwa vijana na wachezaji wa zamani (veterans) ambao wanatumia uwanja huo.
“Tunatarajia kuwasiliana na ofisi ya mkurugenzi wa jiji kuboresha uwanja huu wa Baraa na bahati nzuri afisa michezo amekuwepo leo na kututaka twende jumanne naamini ombi letu litafanikiwa na tutaiboresha kwa ajili ya faiida ya visazizi vijavyo”,Kidungu.
Akizungumzia bonanza la Sabasaba ambayo imeshirikisha timu sita za Mwangaza, AICC Kijenge, KMKM ya Zanzibar, Free Stress ya Dar na Chuo Kikuu cha Nelson Mandela.
Amesema ushindani ulikuwa mkubwa ,ni msimu wa sita wa muchuano hiyo lengo ni kuwaweka pamoja wachezaji wa zamani hada katika kudumisha umoja na mshikamano pia kwa ajili ya kuboresha afya.
Naye Fredrick Lyimo “Deco” ,ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Wilaya ya Arusha Mjini (ADFA), ameipongeza Mwangaza Veterans kwa kwa kuandaa bonanza ambalo limelenga kuwaweka pamoja wachezaji wa zamani lakini pia kurudisha kwa jamii kile ambacho wanakipata.
“Kama uongozi tuko tayari kutoa ushirikiano muda wowote kwa timu zote hapa Arusha lengo letu ni lazima soka hapa Arusha lichezwe”.
Sabasaba bonanza mwaka huu 2025 imekuwa ni timu ya AICC Kijenge kutoka Arusha, mshindi wa pili KMKM Zanzibar na mshindi wa tatu Mwangaza Veterans Arusha.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Arusha
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments