Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Kisasa unaoendelea jijini Arusha, maarufu kama Uwanja wa Samia Suluhu Hassan, umefikia asilimia 51. Uwanja huu unajengwa katika eneo la Olomoti, ambapo kazi ya umwagaji wa zege kwenye muundo mkuu wa jengo imeanza, ikikadiriwa kufikia mita za ujazo 50,000.
Mradi huu mkubwa unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 24, 2026, ukiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027. Ambapo Tanzania ni mwenyeji mwenza sambamba na Kenya na Uganda.
Tanzania inapiga hatua kuhakikisha inakuwa na miundombinu ya kisasa ya michezo. Uwanja huo mpya utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000, na ni moja kati ya viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ya kimataifa. Kukamilika kwake si tu kutakuza michezo, bali pia kutachangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mkoa wa Arusha na Taifa kwa ujumla.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments