Baada ya kufanya kampeni katika zaidi ya mikoa 16 nchini, Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na ziara yake ambapo Septemba 29 amewasili katika Wilaya ya Pangani, Mkoa wa Tanga, ikiwa ni mkoa wa 18 alioufikia tangu kuanza kwa kampeni mwaka huu.
Siku moja kabla, Septemba 28, Dkt. Samia alifanya kampeni zake mkoani Pwani, mkoa wa kimkakati katika kuendeleza mapinduzi ya kiuchumi nchini. Katika hotuba yake, alisisitiza dhamira ya Serikali ya kuongeza thamani ya rasilimali na bidhaa zinazozalishwa nchini kwa lengo la kuongeza tija katika sekta ya viwanda na kuvutia wawekezaji.
Miongoni mwa miradi ya kimkakati aliyoitaja ni pamoja na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Reli ya Kisasa (SGR), na miundombinu ya barabara inayolenga kuunganisha mkoa huo na maeneo mengine muhimu ya kiuchumi.
Lengo kuu la miradi hiyo ni kuimarisha uchumi wa ndani kupitia uongezaji thamani wa mazao na bidhaa, kuimarisha ajira kwa Watanzania, na kuongeza uwezo wa nchi kujitegemea kiuchumi.
Mapokezi makubwa yamemsubiri Dkt. Samia Pangani, ambako wananchi wamejitokeza kwa wingi, wakiwa na shauku ya kusikiliza sera, mikakati na ahadi za CCM kuhusu maendeleo ya wilaya yao na taifa kwa ujumla.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments