DKT. SAMIA NGUZO YA UKOMBOZI WA MWANAMKE WA KITANZANIA

 

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kudhihirisha dhamira yake ya dhati ya kuwawezesha wanawake wa Tanzania kupitia sera zenye mwelekeo wa maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi.

 

Kupitia kampeni zake zinazogusa maisha ya wananchi wa kada zote, Dkt. Samia amekuwa mstari wa mbele kutangaza mikakati ya kuwakwamua wanawake walioko mijini na vijijini kwa usawa.

 

Ni kinara wa kuimarisha Biashara Ndogo Ndogo na Mazingira ya Ujasiriamali kwa Wanawake. Katika ziara yake ya kampeni mkoani Kigoma, wilayani Uvinza, Dkt. Samia alihutubia maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa Tambuka Reli, ambako aliahidi kujenga mabanda ya kisasa kwa ajili ya wanawake wajasiriamali. Hii ni hatua madhubuti ya kupambana na changamoto ya ukosefu wa maeneo rasmi na salama ya kufanyia biashara.

 


“Nataka mwanamke mfanyabiashara wa Kigoma apate nafasi ya kuuza bidhaa zake sehemu salama, safi na inayovutia wateja. Tutajenga mabanda ya kisasa ili biashara zenu zikue na maisha yenu yawe bora,” alisisitiza Dkt. Samia.

 

Afya Bora kwa Wanawake na Watoto ni Kipaumbele cha Serikali ya awamu zake. Rais Samia ametangaza mafanikio ya ongezeko la upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya nchini kutoka asilimia 80 hadi 91. Aidha, ametangaza mpango wa kujenga kituo kipya cha afya katika Kata ya Kazuramimba, hatua itakayowanufaisha zaidi wanawake na watoto wa vijijini kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa ukaribu.

 

Hakurudi nyuma katika suala la Elimu Jumuishi kwa Watoto wa Kike.Kupitia uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Shilingi bilioni 32 katika sekta ya elimu, serikali ya Dkt. Samia imefanikiwa kujenga shule mpya 34 za msingi na kuongeza idadi ya shule za sekondari hadi 3 katika maeneo mbalimbali. Hii ni faraja kubwa kwa akina mama, hasa walioko maeneo ya pembezoni, ambapo watoto wa kike walikuwa wanakosa fursa ya elimu bora.

 

Lakini pia amezingatia suala la Ujuzi ili kurahisisha suala la Ajira kupitia Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana na Wanawake. Hii yote ni katika juhudi za kukuza ajira na kupunguza utegemezi, zaidi ya Shilingi bilioni 2.8 zimetumika katika ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA). Chuo hiki kitatoa mafunzo kwa vijana na wanawake, likiwa ni jukwaa la kuandaa wasichana wengi kuwa na ujuzi wa kujiajiri na kujitegemea.

 

Dkt. Samia hakika ni mama  mwenye upendo wa dhati na Taifa lake, kupitia ruzuku kwa Wakulima na Wafugaji Wanawake wa Vijijini, Dkt. Samia ameendelea kusambaza mbolea na pembejeo za ruzuku kwa wakulima na wafugaji, wengi wao wakiwa wanawake wa vijijini. Hatua hii inalenga kuinua kipato chao na kuimarisha usalama wa chakula, pamoja na kuwapatia fursa ya kujikwamua kiuchumi.

 

Dkt. Samia pia amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza sera na programu zinazowalenga wanawake kwa ujumla, zikiwemo;

 

Mikopo ya 10% ya Mapato ya Halmashauri kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu. Elimu ya Pili kwa Wasichana Walioacha Shule kwa Sababu ya Mimba. Kampeni ya “Building a Better Tomorrow (BBT)” kwa Wanawake Wakulima

 

Uteuzi wa Wanawake Katika Nafasi za Juu Serikalini

Hatua hizi zimemfanya Dkt. Samia kuwa mfano halisi wa uongozi wa kipekee unaolenga kuweka misingi imara ya usawa wa kijinsia.

 

Mwanamke Hakusudiwi Kubaki Nyuma

Kupitia sera na dhamira ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwanamke wa Kitanzania leo anatembea kifua mbele. Kutoka mijini hadi vijijini, matumaini yamechipua. Dkt. Samia si tu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali pia ni sauti ya mwanamke ambaye kwa muda mrefu hakusikika.

 

Katika zama hizi za mabadiliko, ni wazi kuwa Tanzania inaelekea kwenye jamii yenye usawa wa kijinsia, uchumi shirikishi na heshima kwa nafasi ya mwanamke. Akipewa ridhaa ya kuendelea kuongoza, basi ni wazi kuwa, mustakabali wa Watanzania wakiwemo wanawake uko katika mikono salama.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Fatma Jalala

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments