Tafiti zinaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 70 ya ubunifu mpya wa teknolojia duniani unahusishwa moja kwa moja na taaluma ya uhandisi ambayo ndani yake hujumuisha masuala mbalimbali ikiwemo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Nishati, viwanda na akili mnemba.
Hayo yamebainishwa Septemba 25, 2025 jijini Dar es Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alipomwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kufungua Maadhimisho ya 22 ya Siku ya Waandisi kwa Mwaka 2025.
Amesema kuwa Serikali inawahitaji na kuwategemea wahandisi nchini ambao wana fursa ya kuchangia maendeleo ya nchi kupitia utekekezaji wa majukumu yao.
Dkt. Biteko ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya uvumbuzi na maendeleo ya viwanda huhitaji huduma ya wahandisi moja kwa moja.
“ Kwa niaba ya Serikali naomba niwakumbushe kuwa taifa linawategemea sana. Tunawategemea, tunawahitaji naomba mjue Serikali itaendelea kuwategemea wakati wote mnapotekeleza majukumu yenu,” amesema Dkt. Biteko.
Amefafanua kuwa wahandisi hufanya shughuli za ubunifu na uundaji, utafiti na uvumbuzi, usimamizi wa miradi, uhakiki wa usalama na ubora pamoja na ushauri wa Sera na ubunifu wa mifumo mbalimbali duniani kote. Hivyo ni muhimu wajitahidi kuakisi na kutafsiri matarajio yaliyomo katika mioyo ya jamii na kuyaweka katika uhalisia.
Aidha, Dkt. Biteko ameitaka ERB kuwasaidia wahandisi nchini kwa kuwaelekeza na kuwapa mootisha pale wanapofanya vizuri badala ya kubaki kuwa tishio kwao na kuwapa adhabu baada ya kukosea.
Ameendelea kusema motisha kwa wahandisi wazawa walioshiriki katika ujenzi wa miradi ya kimkakati nchini sambamba na kuwapa hamasa na kuwajengea uwezo wa kushiriki miradi mingine ya kimkakati ni muhimu ili kuwapata wahandisi wazalendo
Naye, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa Wizara itaendelea kuimarisha mazingira ya taaluma ya uhandisi ikiwa ni pamoja na kuruhusu mafunzo ya kuongeza viwango vya taaluma hiyo.
Amebainisha kuwa Wizara inaendelea kuhakikisha wahandisi wazawa wanashiriki kikamilifu katika miradi ya kimkakati kama vile SGR. Aidha, ameishukuru Serikali Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujenga miradi ya maendeleo nchini.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Albert Msando akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewaasa wahandisi hao kusimamia taaluma yao katika kutekeleza majukumu yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Menye Manga amesema katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 imetekeleza miradi mikubwa ikiwemo
daraja la Kigongo Busis na wahandisi wengi wa wazawa wameshiriki katika kujenga tofauti na ilivyokuwa awali.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Waandisi (ERB), Wakili Mercy Jilala amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2025 ERB imesajili zaidi ya wahandisi 44,000.
ERB inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwezesha usajili zaidi wa wahandisi hususan wanawake.
Aidha, mkutano huo pia umehudhuriwa na washiriki kutoka nchi za Uganda, Kenya, Ethiopia na India.
Sambamba na maadhimisho ya mwaka 2025 zaidi ya washiriki 4,448 wamehudhuria mkutano huo na wahandisi 400 wamekula kiapo cha maadili ya taaluma hii ya uhandisi.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments