Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Buza zimezinduliwa rasmi Septemba 17, 2025, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Ndugu Ally Mandai.
Akihutubia wakazi wa Kata ya Buza katika uzinduzi huo, Mandai amenukuu kauli maarufu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akisema:
"Wanaweza wakagombea urais wengi sana, lakini RAIS BORA tutampata kutoka CCM!"
Katika hotuba yake, Mandai aliwahabarisha wananchi kuwa mchakato wa kupata wagombea ndani ya CCM huwa ni mgumu na wa kina. Hii ni kwa sababu chama hicho huweka mbele maslahi ya wananchi kwa kuhakikisha kinawateua wagombea bora, wenye sifa na uwezo wa kweli kuwatumikia wananchi.
Ameeleza kuwa CCM ni chama pekee kinachowaleta wagombea wanaokubalika ndani ya chama chenyewe na hata nje ya chama, kwa kuwa kina mfumo madhubuti wa kuchuja na kuandaa viongozi kwa maslahi mapana ya Taifa na wananchi wote.
Mbali na uzinduzi wa kampeni hizo, Mandai pia amezindua rasmi Shina la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwa waendesha bodaboda. Katika hafla hiyo, amewataka vijana hao kushikamana, kuwa na nidhamu, na kutumia kikamilifu fursa zinazotolewa na serikali ya CCM kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na ya jamii kwa ujumla.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments