BILIONI 50 KUBORESHA UPATIKANAJI UMEME HANDENI

 

Dhamira ya dhati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maendeleo nchini inaonekana dhahiri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

 

Aidha, Rais Samia ameweka wazi kuwa utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Handeni mkoani Tanga utakapokamilika utaboresha upatikanaji wa umeme katika Wilaya za Handeni na Kilindi pamoja na maeneo jirani.

 

Rais Samia ameyasema hayo Februari 25, 2025 katika ziara yake mkoani Tanga wakati akizungumza na wananchi wa Handeni mara baada ya kuzindua Shule ya Wasichana ya Kilindi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. 

 

"Tatizo la umeme hapa Handeni Serikali inalifahamu, imeanza kuchukua hatua kwa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kitakachogharimu takribani shilingi bilioni 50 za kitanzania ambacho kitaboresha upatikanaji wa umeme." Amesema Rais Samia.

 

Ameeleza kuwa, upatikanaji wa umeme wa uhakika Handeni utasaidia ukuaji wa uchumi pamoja na kuyainua madini ya kinywe ambayo yanapatikana Wilaya ya Kilindi na yanahitaji umeme wa kutosha.

 

Awali, Mbunge wa Kilindi, Omari Kigua ameishukuru Serikali kwa niaba ya wananchi kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 98 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa gridi imara utakao husisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkata kupitia Handeni hadi Kilindi. 

 

Kigua ameeleza kuwa Wilaya ya Kilindi ina Vijiji 102 ambavyo vyote vimefikiwa na umeme na sasa kazi inayoendelea ni ya kufikisha umeme kwenye Vitongoji.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments