Watumishi wa umma kote nchini wametakiwa kukumbuka
kuwa wamekasimiwa majukumu ya kuwatumikia wananchi na wanatakiwa wasimame katika nafasi zao na kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Maagizo hayo yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Ndugu Sharifa B. Nyanga, Februari 25, 2025.
Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni mara baada ya kufungua rasmi Jengo la Halmashauri hiyo.
Àidha Rais Dkt. Samia ameeleza imani yake juu ya jengo hilo linaimarisha utawala bora na huduma kwa wananchi. Jengo hilo ni moja kati ya majengo 122 yaliyojengwa katika Halmashauri mbalimbali nchini tangu mwaka 2021 ikiwemo jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Bumbuli ambalo Rais Dkt. Samia amelizindua Februari 24, 2025.
Sambamba na hilo Rais Dkt. Samia pia ameweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Miji 28 utakao imarisha upatikanaji wa maji katika Wilaya za Handeni, Korogwe, Muheza na Pangani.
Akiwa Wilaya ya Kilindi, Rais Dkt. Samia ametambua mchango uliotolewa na marehemu Beatrice Shelukindo wakati wa uhai wake katika kutetea haki za wanawake na kupitia nafasi za uongozi alizozishika ikiwemo Ubunge wa Jimbo la Kilindi na Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa heshima yake, Rais Dkt. Samia ameelekeza Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Tanga ipewe jina la Beatrice Shelukindo.
Shule hiyo ambayo imezinduliwa na Rais Dkt. Samia inayojikita kwenye masomo ya sayansi ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kujenga shule 26 za Wasichana katika kila Mkoa kwa lengo la kuimarisha ushiriki wa wanawake kwenye masomo ya sayansi.
Matukio yote haya ni mwendelezo wa ziara ya wiki moja ya Rais Dkt. Samia katika Mkoa wa Tanga, ambapo Februari 24, 2025, Rais Dkt. Samia aliweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji la Mkomazi katika Wilaya ya Korogwe.
Mradi huo unaotarajiwa kuwanufaisha wananchi zaidi ya 20,000 utaimarisha upatikanaji wa maji na kuchochea shughuli za kilimo na uzalishaji wa mazao.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments