DKT TULIA AWATEMBELEA MAJERUHI AJALI ILIYOUA WATU 4 MBEYA

 

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, amewatembelea majeruhi walio nusurika kwenye ajali iliyohusisha gari la serikali na basi la kampuni CRN na kusababisha  vifo vya watu wanne na wengine kujeruhiwa wakiwepo waandishi wa habari.

 

Ajali hiyo ilitokea jana Februari 25,2025 katika kijiji cha Shamwengo ambapo watu saba walijeruhiwa na kukimbizwa Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

 

Dkt. Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ametembelea kuwafariji majeruhi hao wakiwepo waandishi wa habari Epimarcus Apolnali (Chanel Ten), Seleman Ndelage (Dream FM) na Denis George ambaye ni Mwandishi wa kujitegemea.

 


Aidha waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Mwandishi wa kujitegemea, Furaha Simchimba, mjumbe wa kamati ya utendaji wa CCM Wilaya ya Rungwe, Daniel Mselewa na kondakta wa basi ambaye hajajulikana jina lake kwa haraka, huku wengine saba wakijeruhiwa.

 

Dkt. Tulia amewapongeza madaktari wa hosptali ya rufaa kanda na namna walivyotoa huduma kwa majeruhi mara baada ya kufikishwa kutoka eneo la ajali.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments