WANANCHI DODOMA WANUFAIKA NA SERA YA UWEKEZAJI

 

Wananchi wa Dodoma wanaendelea kunufaika na Sera za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo Sera ya Uwekezaji.

 

Aidha, wananchi hao wamenufaika kupitia miradi ya ujenzi wa viwanda mbalimbali ikiwemo upanuzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Cemex kilichopo jijini humo.

 

Uwekezaji wa mradi huo umefikia hatua nzuri, ambapo mashine za kisasa zimewekwa ili kuongeza uwezo wa uzalishaji wa mafuta yenye ubora wa hali ya juu.

 

Kupitia upanuzi huu, wakazi wa Dodoma wataendelela kunufaika kwa njia mbalimbali, ikiwemo fursa za ajira, ujuzi wa kisasa katika kiwanda hiki, pamoja na wakulima wa mbegu za alizeti kupata soko la uhakika kwa mazao yao.

 

Dkt. Furges Antony msimamizi mkuu wa mradi amebainisha hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya Maafisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), waliotembelea kiwanda hicho ili kukagua na kutathmini maendeleo ya upanuzi huo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments