Hali ya Papa Francis inaendelea kuwa mbaya baada ya kukumbwa na tatizo la muda mrefu la changamoto ya kupumua mapema Jumamosi.
Taarifa ya Vatican imesema, Papa "hayuko sawa na alikuwa ameongezewa damu.” ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya BBC Swahili, ni kwamba Vatican ilisema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 88 alikuwa macho na kwenye kiti chake cha magurudumu, lakini alihitaji oksijeni kwa kiasi kikubwa na bado yuko kwenye uangalizi wa hali ya juu.
Papa anatibiwa ugonjwa wa homa ya mapafu katika hospitali ya Gemelli mjini Roma.
Hatua ya kumuwekea damu ilionekana kuwa muhimu kutokana na kiwango kidogo cha seli za damu platelet, inayohusishwa na upungufu wa damu.
Vatican imenukuliwa ikisema "Hali ya Baba Mtakatifu bado ni mbaya,".
Papa ameomba kuwe na uwazi kuhusu afya yake, hivyo Vatican imeanza kutoa taarifa za kila siku.
#KhomeinTvUpdates
✍ Juma Mohamed
🤝🏼BBC Swahili
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments