Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara linawashikilia Mwalimu wa shule ya msingi Nanyani halmashauri ya wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara Mohamed Ally Kajao (34) na Dickson Paul Tamba (27), Mjasiriamali mkazi wa Mkuti chini Machinjioni wilayani Masasi, kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (ASCP) Issa Suleiman, amesema tukio hilo lilifanyika Januari 2025 katika nyumba ya kulala wageni (jina limehifadhiwa) ambapo Dickson Tamba aliruhusu kuingiliwa na Mohamed Ally Kajao, kisha kunakili picha mjongeo (Video) na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Juma Mohamed-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments