NMB, MILLENIUM JOGGING WASAIDIA VYAKULA WAATHIRIKA WA MAFURIKA MTWARA

 

Benki ya NMB Kanda ya Kusini imekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya vyakula wenye thamani ya shilingi Milioni 2, kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyowakumba wakazi wa maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani wiki moja iliyopita.

 


Meneja wa Kanda ya kusini wa benki hiyo Olipa Hebel, baada ya kukabidhi msaada huo Februari 11, 2025 kwa Mkuu wa wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya, amesema benki imeweka vipaombele kusaidia jamii katika majanga mbalimbali.

 


“Tumeweka mikakati mizuri kabisa kuhakikisha katika fedha zetu tunatenga jambo la maafa kuwa ni sehemu ya sisi kushiriki ili kuweza kuwashika mkono wananchi wetu.” Amesema Olipa.

 

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya, baada ya kupokea msaada huo amewashkuru NMB, huku akikiri kuwa na uhitaji zaidi kutokana na ukubwa wa athari zilizojitokeza.

 


“Na ukija kuangalia watu wengi ambao wamepatwa na shida hii, ukute kwa namna mmoja ama nyingine ni wateja wa NMB benki, kwahiyo kwa kutambua mchango huo na nyinyi tunawashkuru sana kwa mchango wenu wa thamani kabisa ambao utakwenda kutatua au kupunguza ile changamoto ambayo wananchi wetu wamepata.” Amesema Mwaipaya.

 


Katika hatua nyingine, wadau wengine ambao ni Klabu ya Mazozi ya Millenium Jogging, nao wamekabidhi msaada kwa ajili ya waathirika hao, wenye thamani ya shilingi Laki Tano, katika ofisi ya mtaa wa Kiyangu.

 


Mwenyekiti wa klabu hiyo Mohamed Sinani amesema “tumeona serikali ya mkoa kupitia Manispaa Mkurugenzi wamekuja nao wametoa na sisi pia tumehamasika tumekuja tumetoa msaada, vilevile kama kuna watu wengine wadau mbalimbali basi tunaomba waje kutoa msaada.” Amesema Sinani.

 


Yusufu Namanolo, ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Kiyangu A, akizungumza baada ya kupokea msaada huo amewashkuru wanakikundi wa Millenium Jogging kwa kuguswa kwao, kisha kuwaomba wahisani wengine kuguswa zaidi na athari za mafuriko hayo kwa kuwasaidia vyakula na mahitaji mengine.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Juma Mohamed-Mtwara

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments