SERIKALI KUPITIA TTCL YADHIBITI UHALIFU MTANDAONI KWA KUTUMIA LAINI ZA SIMU

 



Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti kutokomeza tatizo la matumizi mabaya ya laini za simu, ikiwa ni pamoja na laini za TTCL, zinazotumika katika utapeli.

 

Hayo yamesemwa  Februari 11, 2025 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Marypriscar Mahundi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda.

 

Naibu Waziri Mahundi, amesema hatua zinazochukuliwa ni pamoja na usajili wa laini kwa alama za vidole ili kuhakikisha kila laini inahusiana moja kwa moja na mmiliki wake halali.

 

Aidha, ameongeza kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeanzisha mifumo ya kufuatilia na kufungia laini zinazotumika kwa uhalifu.

 

Vilevile, amesema elimu kwa umma inaendelea kutolewa kuhusu namna ya kutambua na kuripoti matukio ya utapeli kupitia namba maalum 15040.

 

Pia, amesema Serikali inashirikiana na watoa huduma za mawasiliano, wakiwemo TTCL, ili kuhakikisha laini zinazotumika kwa ulaghai zinadhibitiwa mara moja.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments