DAKTARI MZRH AIKABIDHI HOSPITALI MASHINE ZA MATIBABU YA UPUMUAJI KWA WATOTO

 

Daktari Bingwa wa magonjwa ya watoto wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH), Dkt. Angela Leonard amekabidhi mashine mbili  za kutoa dawa  hususani kwa wenye matatizo ya kupumua katika Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH).

 

Dkt Angela amekabidhi mashine hiyo jana Februari 11,2025 kwa Mkurugenzi mtendaji wa Hosptali hiyo Dkt. Godlove Mbwanji ikiwa ni sehemu ya shukrani  kwa hospitali na watumishi wakati wa kutekeleza majukumu yake.

 

Amesema amewiwa kuchangia mashine kama sehemu ya kuboresha utoaji wa huduma kwa watoto walio na changamoto mbalimbali.

 

Mkurugenzi mtendaji wa Hosptali ya Kanda Dkt. Godlove Mbwanji, ameshukuru kwa mchango  mkubwa ambao utasaidia kutoa huduma bora  kwa watoto  wanaokabiliwa na changamoto ya  mfumo wa kupumua. 

 

"Mashine hizi  muhimu katika hospitali yetu zitatumika kutoa huduma bora za matibabu kwa watoto wenye changamoto mbalimbali  wakiwepo  wanaosumbuliwa na magonjwa ya  mfumo wa upumuaji na  mengine .”

 

Dkt. Mbwanji, ameomba na wadau wengine kuwa na  tabia ya kujitoa  kuchangia huduma za afya kama  sehemu ya shukrani ili kupata  baraka ya mafanikio kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

 

Awali, Dkt. Angela, amesema ameamua kutoa mashine ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini.

 

“Naamini kuwa kila mtoto ana haki ya kupata matibabu bora mashine  zitarahisisha mchakato wa matibabu na kuokoa maisha ya watoto wengi, "amesema.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments