Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Machi 25, 2025 amezindua lango la kuingia na kutoka watalii la Ndea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lililopo Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Uzinduzi wa lango hilo ambalo limegharimu Shilingi Milioni 350 ni sehemu ya uboreshaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ili kuchochea na kuongeza vivutio vya utalii nchini.
Akitoa taarifa ya lango hilo Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Emmanuel Mwailama amesema ujenzi wa lango hilo utaongeza idadi ya watalii katika mbuga hiyo ambao wengi wanakwenda kuona maisha ya wanyama pembezoni mwa ziwa Jipe, Faru weusi pamoja na Tembo.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments