RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA DC MASASI|BI. KASANDA AZIBA NAFASI




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Bw. Lauteri John Kanoni, na nafasi yake kujazwa na Bi. Rachel Stephen Kasanda.

 

Katika taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu leo Machi 25, 2025, ni kwamba Rais Dkt. Samia mbali na uteuzi huo wa Mkuu wa Wilaya, amemteuwa Prof. Jafari Ramadhan Kideghesho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania.

 

Aidha, Rais Samia amemteuwa CPA. Ashraph Yusuph Abdulkarim, kuwa Meneja Mkuu wa Shiraka la Masoko Kariakoo.

 

Katika hatua nyingine, Rais Samia amewapangia vituo vya kazi mabalozi Wawili ambao ni Balozi Hamad Khamis Hamad, aliyepangiwa nchini Msumbiji na Balozi Mobhare Holmes Matinyi, aliyepangiwa nchini Sweden.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Juma Mohamed

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments