Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, imetoa wito kwa taasisi kuweka vipaumbele katika kuboresha miundombinu, hasa katika maeneo yenye vyanzo vya kiuchumi kama vile maeneo ya uwekezaji.
Prof. Mkumbo ameyasema haya Machi 25, 2025 baada ya ufunguzi wa ofisi ya Kanda ya Nyasa ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) iliyoko Njombe.
Prof. Mkumbo amezungumza akiwa katika kiwanda cha Murikado Food Supply Co. Ltd, kilichopo Makambako ambacho kinamilikiwa na Mtanzania aliyewekeza kiasi cha shilingi bilioni 5 za kitanzania kinachochakata mafuta ya parachichi mkoani humo.
Amesisitiza kuwa huduma za msingi kama maji, barabara, na umeme ni muhimu mno kwa mwekezaji, ambaye hapaswi kuhangaika kuhusu huduma hizi, kwani anakuja kuzalisha ajira na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa eneo husika.
Ameendelea kwa kumpongeza mwekezaji huyu, ambaye ni Mtanzania aliyewekeza na kuona fursa katika sekta ya kilimo hadi uchakataji wa mafuta. Pia amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafurahishwa kuona Watanzania wajasiri kama hawa wanaothubutu na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments