Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati, Neema Mbuja imesema, kile ambacho wanawake walikipambania katika majukwaa mbalimbali ikiwemo ya Kimataifa ili kuwa na haki, usawa na uwezeshaji kwa wanawake matunda yake yanaonekana hivi sasa.
Hayo yamehabarishwa na Mbuja wakati akieleza safari ya mwanamke katika kudai haki, usawa na uwezeshaji kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo nchini Kitaifa yatafanyika mkoani Arusha.
"Wanawake wengi walipambana kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia, usawa wa utendaji kazi na ushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi na tangu kufanyika kwa Mkutano wa Beijing mwaka 1995 mambo yote ya usawa kwa sasa yanaonekana kwa vitendo." Amesema Mbuja
Ameeleza kuwa Serikali imekuwa kinara katika kuhakikisha haki kwa mwanamke inapatikana.
Ameongeza kuwa, Wizara ya Nishati inajivunia kwa uwepo wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments