TULIA TRUST YATOA MAVAZI KWA WANANCHI WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU


 Taasisi ya Tulia Trust imerejesha tabasamu kwa wazee na watoto wanaoishi  mazingura magumu katika kata sita za Jiji la Mbeya.

 

Tukio hilo limefanyika Machi 23, 2025 na Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Dkt. Tulia Ackson.

 

Akizungumza katika zoezi hilo, Diwani Kata ya Mwakibete ,Lucas Mwampiki amesema Dkt Tulia Ackson amekuwa kiongozi wa kuigwa kwa namna anavyoigusa jamii yenye mahitaji.

 

"Sio hili la leo tu Dkt Tulia amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Mbeya mbali na kutoa mavazi amejenga nyumba za wahitaji, bima za afya na misaada mingine mbalimbalu,"amesema.

 

Wakati huo huo Taasisi hiyo imekabidhi mahitaji kwa familia ya watoto watatu walioshindwa kuendelea na masomo kwa kukosa mahitaji baada ya kufiwa na baba yao mzazi na Mama kuwatelekeza.

 


Familia hiyo iligundulika hivi karibuni wakati Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Dkt. Tulia Ackson kugawa kadi za bima kwa kaya maskini 9,000 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.

 

Miongoni mwa mahitaji ni pamoja na daftari, begi, sare za shule, viatu sambamba na nguo za aina mbalimbali kwa ajili ya kuwasitiri.

 

Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo Mtoto Latifa Emmanuel Mengondele (12) amesema yeye na wadogo zake walikwama kuendelea na masomo kwa kukosa mahitaji baada ya baba yao kufariki na kubaki kumtegemea shangazi yao.

 

"Kabla baba hajafariki Mama alituacha na kwenda kusiko julikana, namshukuru sana Mbunge wetu Dkt. Tulia Ackson kwa kuturejeshea matumaini yaliyopotea na kumuhaidi kusoma kwa bidii ili atimize ndoto yake ,"amesema.

 

Akizungumza kwa niaba ya Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust, Mwangosi Lugano amesema familia hiyo iligundulika hivi karibuni baada ya  Dkt. Tulia kugawa kadi za bima za afya.

 

Amesema familia hiyo ilishindwa kuendelea na masomo kwa kukosa vifaa vya shule jambo lililowafanya kukosa msaada na kuishi nyumbani huku msaada mkubwa ukiwa kwa shangazi yao.

 

"Baada ya baba yao kufariki jukumu la kuwatunza lilikuwa la shangazi yao ambaye alikwama kuwahudumia kutokana na hali ya uchumi,"amesema.

 

Mwangosi amesema mbali na kuisaidia familia hiyo pia wametoa misaada ya mavazi katika kaya zenye wazee na watoto wenye mahitaji maalum  zaidi ya 100  kwenye kata sita.

 

Amesema lengo la Taasisi ni kuzifikia kata 36 za jiji la Mbeya na kuweka bayana nguo zilizotolewa ni sehemu ya michango ya wadau mbalimbali kupitia Taasisi hiyo.

 

Baadhi ya wahitaji wameshukuru Taasisi hiyo kwa msaada huo na kwamba Dkt. Tulia amekuwa akifanya mambo ya kimungu katika kuwatumikia wananchi wa Jiji la Mbeya.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv



Post a Comment

0 Comments