RAIS SAMIA ATUMA SALAM ZA POLE KWA WAFIWA NA MAJERUHI WA AJALI KILIMANJARO

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salam za pole kupitia mtandao wake wa kijami (Whatsapp), kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Mamba Msangeni wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, na kusababisha vifo vya watu Wanane na majeruhi 41.

 

Rais Samia ameandika kama ifuatavyo; “niimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya barabarani iliyotokea Aprili 3, 2025, katika eneo la Mamba Msangeni, Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, na kusababisha vifo vya watu nane na majeruhi arobaini na moja. 

 

Natuma salamu za pole kwa wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali hii. Naendelea kuwasihi watumiaji wote wa barabara kuendelea kuwa waangalifu na kufuata sheria za usalama barabarani. Nasisitiza vyombo vyetu vya usalama barabarani kuendelea kusimamia sheria kwa makini ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika, ikiwemo kufuta kabisa leseni kwa madereva wenye makosa yanayochukua uhai wa Watanzania wenzetu. 

 

Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu ndugu zetu marehemu wa ajali hii wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapate kupona kwa haraka.” Ameandika Rais Dkt. Samia.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments