SILAA ASHIRIKI UFUNGUZI MKUTANO WA KIMATAIFA WA AKILI UNDE, RWANDA

 

Waziri Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa Pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Bw. Kundwe Moses Mwasaga, Aprili 03, 2025 wameshiriki katika kikao cha mawaziri kuhusu matumizi ya Akili Unde ambacho kimefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kigali jijini Kigali, nchini Rwanda.

 

Kikao hicho kimeratibiwa na Taasisi ya Tony Blair (Tony Blair Institute for Global Change - TBI) ambacho kimejikita katika kubainishi namna Akili Unde inavyoweza kutumika na inavyotumika katika maeneo mbalimbali na kuleta ufanisi katika Sekta ya Umma barani Afrika. 

 

Kikao hicho ni sehemu ya Mkutano wa Kimataifa wa Akili Unde Barani Afrika unaoendelea nchini Rwanda kuanzia Aprili 3-4, 2025.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments