DKT. BITEKO AWASILI NCHINI MOROCCO KWA ZIARA YA KIKAZI

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi inayolenga kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili katika Sekta ya Nishati. 

 

Akiwa nchini humo, Dkt. Biteko anatarajiwa kukutana na kuzungumza na mwenyeji wake Waziri wa Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali ambapo watajadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Nishati. 

 


Mara baada ya kuwasili, Dkt. Biteko amepokelewa na Naibu Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu nchini humo, Mhe. Mohamed Ouhmed, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na mwakilishi katika eneo la Morocco, Mhe. Ali Jabir Mwadini. 

 

Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dennis Londo, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa  nishati vijijini (REA), Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments