WALIODAIWA KUTUMWA NA MUNGU KUKATA NGUZO YA TANESCO IRINGA WATUPWA JELA

 

Mahakama ya Wilaya ya Mufindi imewahukumu kulipa faini ya sh 500,000 au kutumikia kifungo cha miezi sita Jela kwa kila mmoja washtakiwa watatu baada ya kukutwa na hatia ya uharibifu wa mali kwa madai wametumwa na Mungu.

 

Miongoni mwa washtakiwa hao waliofanya uhabiribu huo ni Emma Makombe (30), Shujaa Makombe (27) pamoja na Ruby Makombe (32) wote ni ndugu wa familia moja na wakazi wa Kijiji cha Nzivi wilayani hapa Mkoani Iringa.

 


Kesi hiyo ya jinai namba 11416 ya mwaka 2025 ambayo hukumu yake imetolewa Mei 13, 20205 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Benedict Nkomola

 

Aidha amesema washtakiwa hao wanakabiliwa na kosa moja la uhabirifu wa mali chini ya kifungu 326 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 rejeo la mwaka 2022, ambapo wakishindwa kulipa faini hiyo watalazimika kutumikia kifungo hicho.

 


Amesema mahakama imezingatia kifungu namba 27(2) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo katika kutoa Adhabu hiyo.

 

Awali akizungumza kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Wakili Mwandamizi wa Serikali Twide Mangula aliomba Mahakana itoe adhabu kali kwa washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa wengine.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments