ITALIA KUENDELEA KUUNGA MKONO MAENDELEO YA TANZANIA

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Cosato Chumi kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Giuseppe Coppola. 

 

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Mei 20, 2025 katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam. Balozi Coppola ameeleza kuhusu nia ya Serikali ya Italia kuendelea kuunga mkono jitihada za kuleta maendeleo zinazofanywa na Serikali chini ya uongozi mahiri wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Balozi Coppola amebainisha kuwa, Italia iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mkopo wa gharama nafuu wa Dola milioni 281 kusaidia utekelezaji wa Awamu ya nne ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa. 

 

Vilevile, ametabanaisha juu ya kurejeshwa kwa Tanzania katika orodha ya nchi zinazonufaika na mitaji inayowezesha kuboresha elimu ya ufundi stadi, ambapo kupitia mpango huo Tanzania itanufaika na ufadhili wa hadi Euro milioni 20.

 

Katika hatua nyingine, Tanzania na Italia zilikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uchumi wa buluu, uchukuzi na usafirishaji, mawasiliano na teknolojia ya habari, kilimo na ufugaji, ulinzi na usalama pamoja na biashara na uwekezaji.

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments