Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka Jiwe la Msingi la Jengo la Makao Makuu ya CCM Dodoma, tukio hilo limefanyika Mei 28, 2025, Mtaa wa Salmini mkabala na Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC), jijini humo.
Aidha Rais Samia kupitia mtandao wake wa kijamii ameandika, "Tukio hili muhimu ni hatua nyingine inayoakisi ndoto za waasisi wetu na wananchi kwa ujumla, juu ya kuanzishwa kwa CCM. Lengo la waasisi wetu, wanachama na kila Mtanzania ni kuiona CCM inayoendelea kuwa jukwaa la wananchi kuamua hatma yao, na kudumu kuwa madhubuti katika kupanga na kutenda kwa manufaa ya wananchi."
Ameendelea kusisitiza kuwa, wataendelea kuboresha miundombinu si tu katika Makao Makuu hayo mapya ya CCM, bali pia kwenye ofisi zao nchi nzima. Amesema CCM ni mali ya wananchi. Ofisi zitatumika si tu kwa shughuli za chama na utawala, bali pia kama sehemu ya kuwaandaa vijana kujijenga kiuongozi na kimaadili kupitia mafunzo, tafiti, sera, itikadi na mijadala kwa mustakabali wa Taifa letu.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, sambamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Stephen Wassira, Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments