Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande (Mb), amesema kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina mpango wa kuanza ujenzi wa Ofisi ya TRA katika Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, katika mwaka 2026/27.
Naibu Waziri ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Mjini, Zacharia Paulo Issay, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kujenga Ofisi ya TRA katika Wilaya hiyo.
Amefafanua kuwa katika kipindi ambacho hakuna Ofisi ya TRA, shughuli za ukusanyaji wa mapato ya Serikali zinafanyika kwenye jengo iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments