RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA PAPA ROBERT PREVOST

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pongezi kwa Papa Robert Francis Prevost, kwa kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani.

 

Rais Samia ametuma pongezi hizo leo Mei 8, 2025 kupitia mitandao yake ya kijamii, akiandika

 

“Pongezi za dhati kwa Kardinali Robert Francis Prevost, Papa Leo XIV kwa kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani. 

Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninakutakia kila la kheri katika utumishi wako kwa Kanisa na Dunia kwa ujumla. 
Mwenyezi Mungu akusimamie na kukuongoza.”

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Juma Mohamed

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments