TUNAVYOIANGALIA TANZANIA NI TOFAUTI NA WANAVYOIANGALIA AFRIKA - KADOGOSA

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema shirika hilo limefanikiwa kwa asilimia 50 kutekeleza mpango wa dira  ya Afrika 20-63. 

 

Kadogosa amesema hayo Mei 8, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya Rais wa Msumbiji Fransisco Chapo alipotembelea reli ya SGR kutoka Stesheni jijini Dar es Salaam hadi Pugu.

 

Aidha Kadogosa ameweka wazi kuwa, “tunavyoiangalia nchi yetu ni tofauti na wanavyoiangalia Afrika, lakini kikubwa zaidi ujio huu unatuwezesha kushirikiana kibiashara”.

 

Ameongeza, moja kati ya malengo waliojiwekea ni kujenga reli inayoingiliana kibiashara ambayo tayari imeshatekelezwa, 

 

“Rais Chapo amefurahi kuona reli hii ya kisasa imefanikiwa hususani Tanzania."

 

Mkurugenzi huyo wa TRC amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kumleta mgeni wake kuja kujionea reli ya kisiasa inavyofanya kazi.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments