Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeweka msimamo thabiti kuhusu utekelezaji wa Kanuni za Tiketi Mtandao za mwaka 2024, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kisekta katika kuimarisha huduma za usafiri kwa njia ya kidijitali.
Hayo yamethibitishwa katika taarifa iliyotolewa na LATRA Juni 23, 2023, ambayo ilitabanaisha juu ya kanuni hizo zilizochapishwa katika Gazeti la Serikali Na. 20 Januari 12, 2024, zilizowataka watoa huduma wa mifumo ya tiketi kwa njia ya mtandao kuhakikisha wameidhinishwa rasmi na LATRA kabla ya Julai 01, 2025.
Kwa mujibu masharti ya kanuni, huduma za tiketi mtandao zitaruhusiwa tu endapo zitatolewa na mifumo iliyopata kibali kutoka LATRA baada ya kuthibitishwa kwamba imekidhi vigezo muhimu, ikiwemo:
Kuunganishwa na Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji Kodi wa TRA (EFDMS) sambamba na
Kuunganishwa na Mfumo Mama wa Tiketi Mtandao (CeTS) unaoratibiwa na LATRA.
Taarifa hiyo imeweka bayana kuwa watoa huduma ambao hawatakamilisha usajili na kuidhinishwa kufikia Julai 1, 2025 hawataruhusiwa kuendelea na shughuli zao katika soko la usafiri wa abiria kwa njia ya mtandao.
Pia taarifa hiyo imeongeza kuwa, Kwa sasa LATRA inaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wadau mbalimbali wakiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), watoa huduma za mifumo ya tiketi, wamiliki wa mabasi, pamoja na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) ili kuhakikisha utekelezaji wa kanuni unaenda kwa ufanisi, uwazi na kwa manufaa ya sekta nzima ya usafiri.
Aidha, LATRA inawataka wasafirishaji kote nchini kuchukua tahadhari mapema kwa kuhakikisha kuwa wanatumia mifumo ya tiketi mtandao iliyoidhinishwa rasmi, ili kuepuka usumbufu wa kisheria na kiutendaji utakaoweza kujitokeza baada ya muda wa mwisho kupita.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments