RAIS SAMIA AWASILI JIJINI MWANZA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kuzindua rasmi Daraja la Kigongo–Busisi, moja ya miradi mikubwa ya miundombinu nchini.

 

Daraja hilo ambalo limejengwa juu ya Ziwa Victoria, linatarajiwa kuunganisha kwa urahisi na ufanisi mikoa ya Kanda ya Ziwa, hususan mikoa ya Mwanza na Geita, na hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii katika ukanda huo.

 


Shughuli ya uzinduzi itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na kikanda, pamoja na maelfu ya wananchi kutoka mikoa ya jirani waliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

 

Ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi ni sehemu ya dhamira ya serikali ya awamu ya sita ya kuimarisha miundombinu na kuharakisha maendeleo ya Taifa kwa vitendo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments