Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira anatarajiwa kuanza ziara mkoani Geita Juni 16 2025 ambapo atashiriki vikao vya ndani ya Chama ngazi ya Wilaya na Mkoa vitakavyohusisha pia viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Wasira amewasili Juni 15,2025 katika Uwanja wa ndege Mwanza ambapo amepokelewa na viongozi mbalimbali na kisha kupata nafasi ya kumsalimia na kumfariji Mama Getrude Mongella ambaye hivi karibuni ameondokewa na mumewe mzee Silvin Ibengwe Mongella aliyezikwa Mwanza.
Mbali ya kuwa na ziara Mkoa wa Geita ,Makamu Mwenyekiti Wasira pia anatarajiwa kushiriki uzinduzi wa daraja jipya la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Uzinduzi wa daraja hilo ambalo limejengwa katika Ziwa Victoria unatarajiwa kushuhudiwa pia na viongozi mbalimbali pamoja na maelfu ya wananchi wa Mwanza na mikoa jirani.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments