Baadhi ya vijana wanaofanya shughuli ya usafirishaji abiria kwa kutumia Pikipiki maarufu kama bodaboda waliopo Mkoani Mtwara wamesema kuwa kutojitambua kwa vijana ni moja wapo ya sababu inayopelekea kutoaminiwa na kushindwa kutoa maamuzi.
Wameyasema hayo mara baada yakupatiwa elimu na vijana waliojengewa uwezo wa kutatua migogoro na kujenga amani na shirika la cefa ambapo wameomba elimu hiyo iendelee kutolewa ili kusaidia vijana katika kutoa maamuzi.
"Sisi baadhi ya vijana hatujitambui na ndio maana ni ngumu jamii kutuamini sisi katika kutoa maamuzi hivyo tunajukumu la kubadilika". Amesema mmoja wa vijana hao.
Mohamedi Abdallah Chitengu mmoja kati ya wawezeshaji hao amesema vijana wanapaswa kuacha tamaa na kubadilika ili kuepusha dhana ya kuonekana kutokuwa na mchango katika jamii.
Aidha Chitengu amewataka vijana kujituma na kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo mikutano ya vijiji na mitaa ili kujenga umoja na uaminifu katika jamii kwa ujumla.
"Baadhi ya vijana bodaboda wamekuwa na tamaa jambo linalopelekea kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani, hivyo ni vizuri kuchangamkia fursa kwa kushiriki mikutano ya vijiji na mitaa" alisema Chitengu.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments