Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetoa muda wa siku 14 kuanzia Julai 2, 2025 kwa kampuni sita (6) zinazotoa huduma za tiketi kwa njia ya mtandao, ambazo bado mifumo yao ina changamoto, kuhakikisha zinatatua kasoro hizo ili ziweze kuidhinishwa rasmi. Kampuni zitakazoshindwa kutimiza masharti hayo hazitaruhusiwa kuendelea kutoa huduma.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za LATRA jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2025.
Kampuni zilizotajwa kuwa na changamoto kwenye mifumo yao ni: AB Courier Express Limited, Busbora Company Limited, Logix Company Limited, Mkombozi Infotech Company, Sepatech Company Limited, Web Corporation Limited
Kwa upande mwingine, Pazzy amebainisha kuwa hadi kufikia Juni 30, 2025, kampuni tatu (3) tayari zimekidhi vigezo vinavyotakiwa kisheria na sasa zinaruhusiwa kukamilisha taratibu za mwisho ili kupata vibali vyao. Kampuni hizo ni:
Otapp Agency Company Limited, Hashtech Tanzania Limited, Iyishe Company Limited.
Aidha, kampuni mbili za Duarani Innovative Company na Itule Company zimebainika kuwa na changamoto kwenye mifumo yao na zimepewa muda wa siku 7 kutatua changamoto hizo, na endapo zitashindwa, hazitaruhusiwa kutoa huduma, na wateja wao wataelekezwa kwa watoa huduma waliokamilisha masharti ya kisheria.
Pazzy pia ametoa wito kwa watoa huduma wote wa tiketi mtandao kuhakikisha wanatekeleza matakwa ya kisheria kwa kuunganisha mifumo yao na Mfumo Mkuu wa Tiketi Mtandao (CeTS). Hili linahusisha pia kuingiza taarifa zote za mabasi wanayoyahudumia katika Mfumo Jumuishi wa Tiketi Mtandao wa Mamlaka (UTS).
Mamlaka imesisitiza kuwa kampuni ambazo hazipo kwenye orodha ya waliotambuliwa rasmi, hazitambuliki kisheria kama watoa huduma halali za tiketi mtandao.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments