MDAU wa maendeleo anayeiongoza Taasisi ya Udugu Foundation Saidi Omari Mnyeke, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya kugombea ubunge katika jimbo la Kondoa DC mkoani Dodoma, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza baada ya kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Kondoa, Mnyeke amesema amewiwa kugombea ubunge baada ya kufanya utafiti kwa wananchi na kubaini Kondoa inahitaji Mbunge mwenye maono ya kuleta mageuzi kiuchumi, kijamii na siasa safi.
"Nimejitokeza kugombea uwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kondoa kwa sababu wananchi wanahitaji msimamizi wa ilani ya CCM mwenye Maono ya kuwavusha pale walipo Kwa kuwapambania ili wanufaike na fursa zinazotolewa na Serikali, kuwaendeleza kiuchumi pamoja na kukuza pato la Taifa kupitia Rasilimali zilizopo pamoja na kubadilisha Jimbo la Kondoa kuwa kitovu cha Sekta ya Utalii, ufugaji,na Kilimo cha Kisasa," ameeleza Mnyeke.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Kondoa
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments