NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI AJENDA YA DUNIA, TUNAITEKELEZA KWA VITENDO - DKT. KAZUNGU

 

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan kupitia Naibu katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Dkt Khatibu Kazungu Julai 04, 2025 imepokea magari mawili yatakayotumika kwa ajili ya kampeni ya kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

 

Magari hayo ni mpango wa kampeni ya nishati safi ya kupikia 'Okoa Maisha na Mazingira' itakayoendeshwa nchi nzima na Wizara ya nishati kwa kushirikiana na UNCDF.

 

‘’ Ajenda ya Nishati Safi ya kupikia ni ajenda ya Dunia na sisi Wizara ya Nishati tuko tayari kwa utekelezaji ili kumuunga mkono Mhe. Rais Samia’’ Amesema Dkt. Kazungu

 

Aidha, ameishukuru Umoja wa Ulaya, na UNCDF kwa kutekeleza mradi wa Nishati Safi ya kupikia chini ya mfuko wa Cook fund kwa kuwa umesaidia kubadili maisha na mitazamo ya wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi ya Nishati Safi.

 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Balozi wa Umoja wa Ulaya Balozi Christine Grau amesema Umoja wa Ulaya uko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania kwenye utekelezaji wa Nishati Safi ya kupikia na tayari EU imetoa kiasi cha Euro Milioni 19.4 sawa na shilingi Bilioni 59 kutekeleza miradi ya Nishati Safi ya kupikia kwa mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Pwani, Morogoro  na Mwanza. 

 

Kuhusu magari amesema magari hayo mawili yana thamani ya Euro 130,000 na amewataka Wizara ya Nishati kuhakikisha wananchi wa vijijini wanafikiwa na nishati safi ya kupikia

 

Tanzania inajipanga kutekeleza kwa vitendo mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia chini ya mkakati wa Mawasiliano wa Taifa ili kutoa elimu kwa wananchi na kufikia lengo la Serikali la asilimia 80 ya Watanzania kuanza kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments