TANESCO YAPEWA KONGOLE IRINGA

 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepewa kongole na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James kwa juhudi za Shirika hilo katika kuboresha huduma ya umeme mkoani humo.

 

Kongele hiyo imetolewa wakati wa ziara ya kikazi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Lazaro Twange wakati wa ziara yake Mkoani Iringa Julai 22, 2025, James amesema, hali ya upatikanaji wa umeme kwa sasa ni ya kuridhisha inayopelekea mchango mkubwa kwa maendeleo ya wananchi.

 

“Hali ya upatikanaji wa umeme kwa sasa ni tulivu na ya kuridhisha.Tunatoa pongezi kwa TANESCO kwa huduma bora, ushirikiano mzuri, na utoaji wa taarifa kwa wakati,” amesema Kheri James.

 

Katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, ameeleza kuwa lengo la ziara yake ni kukagua maendeleo ya Mradi wa TAZA, mradi wa kimkakati unaolenga kuunganisha Tanzania na Zambia kupitia njia ya kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Sumbawanga, ambao hadi sasa ujenzi wa njia ya usafirishaji umefikia asilimia 67 ya utekelezaji. Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya takribani trilioni 1.5.

 

“Nimekuja kukagua maendeleo ya Mradi wa TAZA ambao unaanzia hapa Iringa hadi Sumbawanga. Mradi huu ni wa kimkakati na tunatarajia kuwa njia hii ya kusafirisha umeme itaunganisha Tanzania na Zambia,” amesema MD Twange.

 

Katika kuendeleza kampeni ya “Umeme ni Nishati Nafuu Zaidi Jikoni”,  Twange amemkabidhi Mkuu wa Mkoa pamoja na Katibu Tawala Doris Kalasa majiko yanayotumia umeme kidogo, na kusisitiza umuhimu wa kutumia umeme kama Nishati Safi ya kupikia nyumbani.

 

“Moja ya ajenda ya TANESCO ni kuhamasisha matumizi ya umeme kama Nishati Safi ya kupikia. Tunaomba viongozi waendelee kuelimisha wananchi kuhusu faida za majiko haya ili waweze kuyatumia majumbani,” amehimiza.

 

Mkurugenzi Twange yupo Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi ya siku mbili ambayo inahusisha ukaguzi wa miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa Mkoani humo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments