AWESO AKOSHWA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI MTO KIWIRA

 

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema ameridhishwa  na utekelezaji  wa ujenzi  wa mradi  mkubwa wa kimkakati  kutoka  chanzo  cha Mto Kiwira  Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya. 

 

Waziri huyo ametoa  kauli  hiyo jana Jumatano  Julai 23,2025  mara baada ya kufanya ziara yake ya kikazi  ya kukagua  utekelezaji  wa mradi huo unaosimamiwa na Mamlaka  ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya (Mbeya Uwsa)na kujengwa  na mkandarasi wa kampuni ya China Rarway Construction Engineering Group  chini ya Mhandisi mshauri GkW Consult GmbH. 

 

Amesema ameridhishwa  na hatua ya utekelezaji  wake huku akimtaka mkandarasi  kuongeza nguvu ya usambazaji wa mabomba na nguvu  kazi.

 

"Niwape pongezi kubwa Mkuu  wa Mkoa,Bodi ya Maji Mbeya Uwsa  na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa usimamizi  mzuri wa ujenzi wa mradi huu mkubwa wa kimkakati, "amesema.

 

Pia Waziri Aweso amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Beno Malisa kufuatilia  utekelezaji  wa miradi ya maji ukiwepo wa miji 28 Wilaya ya Mbarali na kuchukua hatua  kwa watakao kwamisha.

 

Aweso pia katika  ziara yake ametembelea mradi wa miji 28 katika  eneo la Rujewa Wilaya  ya Mbarali  utakao gharimu  sh 130 bilioni  kutokana na fedha za ufadhiri  wa Serikali ya India.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa amemuomba Waziri Aweso kuona namna ya kuboresha  miradi 15 inayotekelezwa na Wakala wa Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) ili kuondoa changamoto  ya maji kwa wananchi. 

 

Mkurugenzi  wa Mamlaka  ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya (Mbeya -Uwsa )CPA Gilbert Kayange  amesema mradi wa chanzo mto Kiwira  umefikia asilimia 45 utakamilika Desemba  mwaka huu 

 

Amesema mradi huo utagharimu zaidi ya Sh bilioni 119 na kuzalisha lita 117 milioni kwa siku na kupelekea ongezeko la upatikanaji  wa huduma kwa wananchi wa Mji wa Mbalizi na Mkoa wa Mbeya. 

 

Mkazi wa Kiwira  Subira Mwakyusa amesema hiyo ni fursa kwao katika kuondokana na hadha iliyopo katika baadhi ya maeneo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments