Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeonesha dhamira thabiti katika kuimarisha usalama wa mtandaoni kwa kuzindua kampeni ya elimu kwa umma kuhusu utapeli wa mtandaoni iitwayo "SITAPELIKI".
Kampeni hii inayosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) kwa kushirikiana na watoa huduma wa makampuni ya simu za
mkononi, inalenga kuwaelimisha wananchi juu ya mbinu za kujilinda dhidi ya matapeli wa mtandaoni.
Uzinduzi wa kampeni hii umefanyika jijini Arusha na unatarajiwa kuwa na matokeo chanya kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini.
Hii ni hatua nzuri kwa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuchukua hatua madhubuti katika kulinda wananchi dhidi ya uhalifu wa mtandaoni na kuhakikisha teknolojia ya mawasiliano inabaki
kuwa salama na yenye manufaa kwa jamii yote.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments