Kijana mwenye maono na ari ya kulitumikia Taifa, Deogratias Kimoso amechukua rasmi fomu ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam, Juni 28,2025 ikiwa zoezi hilo limefunguliwa rasmi leo na kutarajiwa kumalizika tarehe 2, Julai, 2025.
Tukio hilo limefanyika katika ofisi za chama cha Mapinduzi - CCM Wilaya ya Kigamboni, ambapo Kisomo amekabidhiwa fomu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu, Deogratias Kimoso amesema ameamua kujitosa katika siasa kutokana na msukumo na dira ya Rais Samia, ambaye amekuwa akisisitiza ushiriki wa vijana katika maendeleo ya Taifa.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa siasa, ongezeko la vijana kuchukua fomu za kugombea mwaka huu ni dalili ya kuongezeka kwa hamasa ya kisiasa miongoni mwa kizazi kipya, hali inayochangiwa pakubwa na uongozi wa Rais Samia unaoweka mkazo katika usawa wa kijinsia, uwakilishi wa vijana, na maendeleo jumuishi.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments