DKT. TULIA AFUTURISHA WANANCHI 1,800 MBEYA

 

Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson amewafuturisha Wananchi 1,800 wa jijini Mbeya wakiwamo waumini wa dini ya Kiisilamu na viongozi wa chama na serikali.

 


Akizungumza kwenye hafla hiyo ya Iftari iliyofanyika Machi 27, 2025 Dkt,Tulia amewashukuru waumini na wananchi waliojitokeza kushiriki kwa ajili ya kumshukuru Mungu katika mfungo unaoendelea.

 


Pia Dkt ,Tulia ameomba watanzania kuendelea kuliombea taifa katika kuelekea uchaguzi Mkuu hususani Rais Samia Suluhu Hassan.

 


"Niwaombe tuendelee kufanya dua kumuombea afya njema Rais Samia Suluhu Hassan Mungu amlinde afike Oktoba 2025 katika uchaguzi Mkuu na kufafanua kuwa ameleta maendeleo makubwa katika Mkoa wa Mbeya.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments