SERIKALI YATOA MIEZI MIWILI BARABARA ZA TARURA IKWIRIRI ZIKAMILIKE

 

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, imemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Leopold Runji, kuhakikisha wakandarasi wanakamilisha ujenzi wa barabara za lami Ikwiriri ndani ya miezi miwili ili wananchi wanufaike na maboresho ya miundombinu hiyo.

 


Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo wilayani Rufiji.

 

 "Natoa miezi miwili tu, barabara ziwe zimekamilika ifikapo Mei 30, 2025, ikiwa ni pamoja na mitaro na taa za barabarani. Hakutakuwa na nyongeza ya muda," amesisitiza Waziri Mchengerwa.

 


Amemuagiza Meneja wa TARURA kuwasimamia wakandarasi wafanye kazi usiku na mchana, akibainisha kuwa barabara hizo zilipaswa kukamilika Desemba 2024 na iwapo hazitakamilika kwa muda uliopangwa, atamuwajibisha meneja huyo.

 


Nao, Baadhi ya wananchi, akiwamo Dereva wa bodaboda Ramadhan Mwipi na Mama Lishe Mariam Hamza, wamemshukuru Waziri Mchengerwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha barabara hiyo, wakieleza kuwa imeleta ahueni kubwa kwa usafiri na biashara zao.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments