Rais Haikainde Hichielema wa Zambia amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujumbe maalum uliowasilishwa kwake na Waziri wa Afya Jenista Mhagama. Rais Hichielema amebainisha kuwa Zambia na Tanzania ni nchi zenye historia na ushirikiano wa kindugu muda mrefu na usio na mipaka.
Machi 24, 2025 Waziri wa Afya Jenista Mhagama aliwasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Haikainde Hichielema katika Ikulu ya Rais iliyopo Jijini Lusaka Zambia.
Waziri Mhagama akiwa ameambatana na ujumbe wake akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Zambia Luteni Generali Mathew Edward Mkingule amemshukuru Rais Hichielema kwa mapokezi mazuri na ushirikiano imara ulipo baina ya Tanzania na Zambia.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments