Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi wameshauriwa kujifunza kuhusu uwekezaji mapema ili kuhakikisha kuwa baada ya kustaafu wanaendelea kuishi maisha mazuri, kama walivyokuwa kazini.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Masoko Mwandamizi, Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS, Rahim Mwanga, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa kwa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Mwanga amesema kuwa, kustaafu hakupaswi kuwa chanzo cha matatizo ya kifedha, kwa mfanyakazi yoyote aliyekuwa analipwa mshahara bali iwe fursa ya kufurahia matunda ya kazi ya muda mrefu.
“Tukijijengea utamaduni wa kuwekeza mapema kutatusaidia sisi wafanyakazi kuepuka changamoto za kifedha baada ya kustaafu na kuwa na maisha ya uhakika”, amesema Mwanga.
Aidha amewasisitiza wafanyakazi wote nchini kuhakikisha michango yao inalipwa kwa wakati na waajiri wao lakini pia watumie Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inayotoa faida kubwa.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Erick Mvati, ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kufika katika Mkoa wa Mwanza kutoa elimu ya fedha ambayo ni muhimu kwa wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Sambamba na Msimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Santley Kibakaya, amesema, Wizara inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi ili wafahamu fursa mbalimbali zinazopatikana katika Sekta ya Fedha.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments