Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imezitaka Taasisi za Fedha zilizosajiliwa kutoa huduma ya mikopo, kuto wakandamiza wananchi katika mikataba kwa sababu ya kutojua kusoma na kuandika kwa kuwasainisha mikataba bila uelewa wao.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza, Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija, alipokutana na Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, ambayo ipo mkoani Mwanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali.
“Serikali imesisitiza umuhimu wa uwazi na haki katika mikataba ya kifedha ili kulinda haki za wananchi na kuhakikisha wanajua kikamilifu masharti wanayokubaliana nayo”, amesema Ludigija.
Amefafanua kuwa Serikali inatambua kuna baadhi ya wananchi hawajui kusoma na kuandika, wamekuwa wakiwekewa miezi mingi zaidi ya marejesho tofauti na walivyokubaliana kwa mdomo.
Ludigija amewashukuru wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kufika mkoani Mwanza kutoa elimu ya fedha kwa kuwa itawasaidia wananchi kuwa na uelewa mpana wa masuala ya fedha ikiwemo kupanga bajeti na kufanya uwekezaji ambao utakuwa na faida kwa kujikwamua kiuchumi.
Afisa Mkuu Mwandamizi, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, amewasisitiza wananchi kujenga mazoea ya kusoma mikataba na kuielewa kabla ya kusaini.
Ameongeza kuwa baadhi ya wanufaika wa mikopo wanakumbwa na changamoto za marejesho kwa sababu ya kukosa mipango thabiti ya matumizi ya fedha wanazokopa, na wengine hawasomi wala kuelewa mikataba wanayoingia.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha, mkazi wa Kwimba, Nkwadi Joseph ameishukuru Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaletea wataalamu wa fedha.
"Kabla ya kupata elimu hii, tulikuwa tunaingia kwenye mikopo yenye masharti magumu bila kujua athari zake, sasa tunaelewa umuhimu wa mikopo yenye utaratibu mzuri," amesema Joseph.
Serikali kupitia Wizara ya Fedha imefanya hitimisho ya kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali katika Wilaya za Ilemela, Magu, Misungwi na Kwimba Mkoa wa Mwanza, ambapo hadi sasa Wizara ya Fedha imeshatoa elimu ya fedha katika mikoa 16.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments