Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Meshack Anyingisye, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu – El Maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Czech, uliongozwa na Balozi wa Czech nchini Kenya, Nicol Adamcova, katika ofisi za Wizara ya Fedha, Jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine, yalilenga utiaji saini wa Mkataba wa kuondoa utozaji Kodi mara mbili kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Czech ambao unatarajiwa kuweka mazingira ya kodi yanayotabirika ili kuvutia uwekezaji wa mitaji ya muda mrefu pamoja na kuondoa mzigo kwa wawekezaji wanaoendesha shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Kamisha Msaidizi wa Sera, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia masuala ya kodi za Kimataifa, Juma Mkabakuli.
Nchi hizi mbili zilikamilisha majadiliano ya Mkataba wa kuondoa utozaji kodi mara mbili mwaka 2024 na kwa sasa taratibu zote za kisheria za ndani kwa nchi zote mbili zimekamilika kwa ajili ya kusainiwa mkataba huo na kuanza utekelezaji.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments