SERIKALI YABORESHA MIUNDOMBINU YA UMEME KIBITI

 

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inatekeleza miradi mbalimbali ya matengenezo na ukarabati wa njia za kusafirisha na kusambaza umeme katika Wilaya ya Kibiti ili kuondokana na tatizo la kukatika kwa umeme kunakotokana na uchakavu wa miundombinu hiyo.

 

Kapinga ameyasema hayo Mei 12, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti, Twaha Mpembenwe aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali kutatua tatizo la kukatika kwa umeme Jimbo la Kibiti. 

 

Ameitaja Mikakati hiyo ni kubadili nyaya za umeme kwa kuweka zenye uwezo mkubwa, kubadili nguzo za umeme na kuweka za zege, kubadili 'Pin insulators' na kuweka mpya, na kufunga vidhibiti matatizo (fault auto recloser) kwenye line zenye urefu wa zaidi ya Kilomita 50.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments