Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Juni 28,2025, amezindia kiwanda kikubwa cha mbolea cha ITRACOM Fertilizers Limited jijini Dodoma.
Katika uzinduzi huo, Rais Samia ameshirikiana na Rais wa Jamhuri ya Burundi, Évariste Ndayishimiye. Hili ni tukio la kihistoria linalodhihirisha dhamira ya pamoja ya kukuza uwekezaji wenye manufaa kwa pande zote mbili.
Aidha Rais ameandika katika mitandao yake ya kijamii kuwa, "jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali katika kipindi cha miaka minne kilizopita hususan kuboresha sera, sheria na kuvutia uwekezaji zinaendelea kuzaa matunda." Rais Samia.
“Kiwanda hiki, ambacho ni kikubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki, kinathibitisha nia ya dhati ya nchi zetu ya kukuza uwekezaji unaogusa maisha ya watu. Vilevile, kinaongeza chachu katika mageuzi ya kilimo, tunayoyaendeleza, ikiwa ni pamoja na kuongeza matumizi ya mbolea ili kukuza uzalishaji, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza mchango wa kilimo katika uchumi wa taifa letu,” amesema Rais Samia.
Ameongeza kuwa uwekezaji huo mkubwa unatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja takribani 3,000, hatua inayosaidia kupunguza ukosefu wa ajira hasa kwa vijana.
Vilevile Rais Samia ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa usambazaji wa mbolea unafika hadi vijijini ili wananchi waweze kuona manufaa halisi ya uwekezaji mkubwa unaofanyika ndani ya nchi yao.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments