VIJANA KIGAMBONI WADHAMIRIA KUMSAIDIA RAIS SAMIA KUPITIA NAFASI YA UBUNGE

 

Katika kile kinachoonekana kuwa ni mwamko mpya wa kisiasa miongoni mwa vijana wa Tanzania, kundi kubwa la vijana kutoka Jimbo la Kigamboni limetangaza nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao, likilenga moja kwa moja kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ajenda yake ya maendeleo kwa vitendo.

 

Vijana hao waliojitokeza Juni 28,2025 ni Ally Mandai ambaye ni Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi - CCM, Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa, Mchumi wa Kamati Kuu ya Fedha Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM.

 

Wengine ni Godfrey Maduhu, Allan Sanga Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa, Mdalaloy Mwinchumu, Mtindi Aman Kabourou, Abubakar Ally, Fridolinus  Mushobozi, Wengine ni Doto Rwaikiza, Cynthia Henjewele na Luca Neghesti ambaye ni mume wa mwanamitindo na mrimbwende wa Tanzania na Dunia wa Afrika mwaka 2005.

 

Vijana hao wameeleza kuwa wanavutiwa na uongozi wa Rais Samia, wakimtaja kuwa ni kiongozi mwenye maono ya kweli kwa Taifa, ambaye ameweka msingi madhubuti wa kujenga uchumi jumuishi, unaogusa makundi yote, hususan vijana.

 

Kigamboni, ikiwa ni moja ya majimbo ya kimkakati jijini Dar es Salaam kutokana na ukuaji wake wa kasi kiuchumi na kijiografia, limekuwa kitovu cha fursa kwa vijana.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments